198. Bariki Yote Yawe Mema

1.  Bariki yote yawe mema,

    yote yawe mbaraka. 

    Watu wa nchi za dunia, 

    uwajaze utukufu.

    Kaa kwetu, Bwana, bariki. 

    Uamini, wee ee ndugu 

    kweli yake Kristo. 

    Jaa utukufu wa Bwana

    siku zako zote. 

        /:Vaa Mwokozi ee 

         na kweli yake, Haleluya./:


2.  Nyumba za wote zibariki

    kwa Jina lako takata. 

    Ujaze utukufu wako,

    nchi zote za dunia,  

          Kaa kwetu, Bwana …


3.  Nyosha mkono ubariki,

    waliojiunga nawe. 

    Wakupokee maishani,

    watunzwe nawe milele. 

            Kaa kwetu, Bwana …


4.  Bwana yatunze mambo yote

    yaliyo mazuri kwako 

    Uwape wote wakuombao,

    wafanikishe maisha.

            Kaa kwetu, Bwana … 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima