180. Bwana, u sehemu yangu
1. Bwana, u sehemu yangu,
Rafiki yangu, Wewe;
katika safari yangu
nitembee na Wewe.
Pamoja na Wewe,
pamoja na Wewe,
katika safari yangu
nitembee na Wewe.
2. Mali hapa sikutaka
ili niheshimiwe,
heri nikute mateso
sawasawa na Wewe.
Pamoja na Wewe,
pamoja na Wewe,
heri nikute mateso
sawasawa na wewe.
3. Niongoze safarini,
mbele unichukue.
Mlangoni mwa mbinguni
niingie na Wewe.
Pamoja na Wewe,
pamoja na Wewe,
Mlangoni mwa
mbinguni
niingie na wewe.
Comments
Post a Comment