214. Tokea Nuru ya Mchana

1. Tokea nuru ya mchana, 

   uamshe mwili na roho

   kwa mwanga wako mzuri.

   Tokea nuru ya roho,

   niimbe wimbo wa sifa 

   wa kumshukuru Mungu. 

   Mwimbieni kwa furaha

   Mwenye enzi alindaye

   na kuwabariki watu.


2. Ninakushukuru Mungu

   kwa moyo wote sababu 

   ya neema yako kubwa.

   Umenilinda usiku

   mwili na roho vizuri 

   kwa jeshi la malaika. 

   Nikaweza kuondoka 

   kitandani kwa furaha 

   mwenye nguvu na uzima.

 

3. Ninakuomba Babangu,

   uyaondoe makosa,

   hofu na shida kwangu. 

   Niamke hata rohoni,

   kwa neema yako na pendo

   nitakutumikia.

   Niongoze nifikiri,

   mambo yangu mbele yako,

   nipate baraka yako.


4. Ee Yesu, uniongoze

   nishike njia yako tu 

   maisha yangu yote. 

   Ulinde mwili na roho

   uangalie mwenendo 

   nisianguke leo.

   Mpenzi wangu, nifundishe, 

   nikumbuke pendo lako, 

   nisishindwe na dunia. 


5. Unitawale kwa roho 

   unionyeshe mwenendo 

   kwenda kwako mbinguni.

   Unibariki popote

   katika kazi na raha,

   nipe riziki yangu.

   Mpaka mwisho 

   niondoke duniani kwa furaha,

   nikushukuru mbinguni.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima