171. Nimepita Ulimwengu
1. Nimepita ulimwengu,
ulimwengu ni mzuri,
lakini natamani
ulimwengu mwingine.
2. Nimeona watu wengi,
hutafuta daima,
Maisha yao yote,
ndiyo taabu na shida.
3. Imebaki hali njema
ya furaha ya roho:
Hubirini pote pote;
taabu itatulia.
4. Msalabani pa Golgota
jerahani mwa Yesu
ni mahali penye raha
kwao wote kabisa.
Comments
Post a Comment