220. Naamka Mimi Tena

1.  Naamka mimi tena 

    kwa nguvu na afya.

    Na moyo wangu Baba, 

    wakusifu wewe.


2.  Baraka na furaha 

    popote zimejaa,

    zatoka kwako wewe 

    zimetuingia.


3.  Twaimba sifa zako

    kwa mioyo na vinywa,

    miti, wanyama wote, 

    wakusifu Bwana.


4.  Na sisi twapaliza 

    sauti zetu sasa,

    maisha yetu yote

    yawe sifa pia! 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima