199. Nikifa Nitapata Uzima kwa Yesu
1. Nikifa nitapata
uzima kwa Yesu.
Ninampa moyo wangu,
nife kwa furaha.
2. Napenda kwenda pale
alipo Bwanangu,
nikae mjini kwake
siku za milele.
3. Nimeushinda sasa
uchungu na woga,
kwa damu ya Mwokozi
nimekombolewa.
4. Zikipunguka nguvu,
pumzi ikiisha,
nisaidie Bwana,
nilale kwa raha.
5. Saa yangu ikifika,
niiache dunia,
unitulize Bwana,
nichukue kwako.
6. Nikifika mbinguni,
nitakuimbia
na kukusifu Bwana,
kwa furaha kubwa.
Comments
Post a Comment