169. Rafiki Bora Yu Mbinguni
1. Rafiki bora yu mbinguni,
duniani rafiki haba,
sababu hapa mapatano
yanavunjika upesi.
Kwa hiyo mimi nasema:
Rafiki bora ni Yesu.
2. Dunia ni kama utete!
Yesu ni Mwamba wa nguvu.
Ningeachwa na watu wote,
Yeye haniachi kamwe.
Kwa hiyo …
3. Maisha yake ametoa,
nami ninajitoa kwake.
Anipenda bila kuchoka,
ashinda hata kaburi.
Kwa hiyo …
Comments
Post a Comment