156. Umejengwa Juu Yerusalemu

1. Umejengwa juu Yerusalemu,

   ninakutamani.

   Moyo wangu ukikutamani, 

   wataka kupita milima na

   mabonde, kuruka kama tai, 

   uache ulimwengu 

   uingie kwako. 


2. Siku nzuri! Ninaingojea, 

   ifike upesi.

   Niiache dunia niende 

   mbinguni kwa shangwe.

   Nimrudishie roho 

   Mwokozi Bwanangu, 

   aipokee vema, aipe uzima.


3. Mara moja roho itakwenda

   kufika mbinguni,

   ikiacha uzima wa hapa 

   kwa nguvu ya Mungu.

   Yapelekwa na gari 

   kama Eliya mkuu, 

   malaika waibeba 

   vizuri kwa shangwe.


4. Nikifika kule Paradiso, mwisho

   huu ni mwema. 

   Roho yangu yajaa furaha,

   kinywa husifu tu.

   Wateule huimba 

   nyimbo nzuri nyingi, 

   hawaachi kumsifu 

   Mungu Mwenye enzi. 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima