160. Maisha ya Duniani
1. Maisha ya duniani ni mafupi,
hata siku ni chache;
zinapita hima na kutoweka
wala hazirudi, zinatokomea.
2. Vivi hivi kila mmoja
tunakwenda
mbinguni kwake Mungu,
mbele ya kiti chake
cha hukumu
kila mtu atapewa haki yake.
3. Tunakwenda huko sote
na waamini
waamini waenda bila woga
kwani wanaye Bwana
wanaiingia nchi takatifu.
4. Ee ndugu, twendeni sote
kwake Mungu.
Ulimwengu wapita;
utaangamia na dhambi zako,
usipokubali nawe waangamia.
5. Basi ndugu tujikabidhi
kwa Mungu tuwapo bado hai;
kwani tukipuuza tutapotea,
hatutaepuka hukumu milele.
Comments
Post a Comment