173. Yesu Mkononi Mwako
1. Yesu mkononi mwako
nitalindwa vema.
Raha bora napata
kwa upendo wako.
Nawe kwa sauti tamu
waniita mimi:
Wacha tu nguvu yako,
kwangu ni raha kuu.
Yesu mkononi mwako
nitalindwa vema,
raha bora napata
kwa upendo wako!
2. Yesu mkononi mwako
sioni taabu.
Shetani nguvu zake
haziwezi kwako.
Shaka na woga kwako
zinakosa nguvu,
na majaribu yote
nayashinda pia.
Yesu mkononi …
3. Umenifia Bwana,
nakukimbilia.
Wanishika milele,
nakutegemea.
Nakungojea hapa
na giza liishe,
mchana wapambazuka
na kwako milele.
Yesu mkononi …
Comments
Post a Comment