Posts

140. Tumsifu sisi Watu

1. Tumsifu sisi watu, tumsifu Mungu Baba, aliyeumba vyote kwa nguvu yake kuu. Wazima watu wote, na ndege wa angani wanyama wa mwituni, kwa huruma yake. 2. Tumsifu sisi watu, tumsifu Bwana Yesu, aliyetukomboa kwa damu yake tu. Amani tumepewa, hatuna hofu tena Ametuhurumia, Mwokozi ni yeye. 3. Tumsifu sisi watu, tumsifu Roho, ndiye Mtulizaji popote, furaha iwe kuu. Moyo umetulia, amani umepata, wamwombao yeye.

141. Tumpeni Sifa na Tukuzo

Tumpeni sifa na tukuzo, sifa na tukuzo ni zake, Ukuu na nguvu zote zimpasaye Mungu, ni vya Bwana, ni vya Bwana  na vimtii siku zote. Tumpeni sifa na tukuzo,  sifa na tukuzo ni zake.  Sifa, maombi na  nguvu zote ni za Bwana  siku zote, kale yote  hata itakayokuja.  Amen. Amen. 

142. Vyenye Uzima Vimtukuze

Vyenye uzima vimtukuze, vimtukuze Bwana,  vimtukuze, vimtukuze,  vimtukuze,  hata na utakatifu wake.  Kwani ameumba mbingu  na nchi.  Vyenye uzima vimtukuze,  vimtukuze Bwana,  vimtukuze Bwana,  vimtukuze Bwana, vimtukuze Bwana.  Na magunda na mazeze  na filimbi na vilangwi  na vinanda  na vimtukuze!  Vyenye uzima na viimbe,  vimtukuze Bwana!  Na magunda na vinanda  Vyote vimtukuze  ee Bwana wa majeshi!  Haleluya!

143. Utukufu ni wa Mungu

Utukufu ni wa Mungu juu,  tukuzo lote, uwezo wote ni wa  Mungu, Bwana wetu, Bwana wetu,  Mungu ni wa pekee  Shangilio lake lijaze katika dunia  popote,  Jina lake litukuzwe na watu wote. Tumshangilie Mungu wetu  na Bwana wetu  nyimbo za tukuzo  Tumpeni heshima zote,  tumwimbie,  Sifa na tukuzo zampasa,  zote ni zake Mungu wetu! 

144. Bwana, Bwana Ndiye Mtakatifu

Bwana, Bwana ndiye  mtakatifu,  anayo nguvu na sasa aliyeko,  na ajaye,  Bwana! Bwana! Mungu,  Mfalme, mwenye uwezo!

145. Bwana Wema Wako Popote

Bwana wema wako popote  hata mbinguni huko juu. Bwana  wema wako popote hata  mbinguni huko juu.     /: Na welekevu, na         welekevu/: wako huenea na  mawinguni  na walekevu wako  huenea na mawinguni.       /:Haleluya x 4       Haleluya x 2/: 

146. Mwenyezi, Mwenyezi, Mwenyezi

Mwenyezi, Mwenyezi, Mwenyezi,  Jina lako litukuzwe sana.  Amin, Amin.  Hata ulimwengu wetu uteketezwe kwa moto.  Nazo nyumba zetu,  ziimbe utakatifu wake,  Haleluya, Haleluya.