225. Mchunga Wangu Mwema

1. Mchunga wangu mwema, 

   huna usingizi unakesha tu.

   Baba, nimeona 

   neema yako leo 

   mchana kutwa huu.

   Hata na usiku huu 

   utawatuma malaika, 

   wanilinde mimi.


2. Uwalinde tena

   baba na mamangu, 

   nao ni wako. 

   Utufiche sisi

   mikononi mwako,

   tusiogope!

   Njoo Bwana, tuungane:

   mimi kwako, nawe kwangu

   hivyo nitalala.

 

3. Linda mlango wangu

   na huzuni zangu niondolee.

   Unikumbatie ndani ya

   mabawa yako nilale. 

   Unifiche vizuri:

   ndivyo mwovu hataweza 

   kunikaribia.


4. Baba, ukitaka 

   kuniita mimi leo usiku,

   nitaweka roho 

   mikononi mwako uipokee.

   Nitalala kwa raha, 

   kwani wewe wanilinda 

   leo hata kesho.


5. Sasa nitalala

   kitandani mwangu

   kwa furaha tu. 

   Roho na maisha 

   nimeweka kwako,

   mlinzi ni wewe.

   Kwa heri unilinde!

   Kama ninaamka kesho, 

   wewe huniachi


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima