223. Jioni Moyo Wangu Wakutafuta

1. Jioni moyo wangu 

   wakutafuta Bwana, 

   na kukushukuru. 

   Unikazie macho 

   yenye baraka nyingi, 

   ung’aze mwili na roho.


2. Natumaini tena 

   rehema yako Baba 

   hata usiku huu. 

   Fukuza majaribu 

   na hila ya Shetani,

   ukiwa karibu yangu.


3. Unanipenda sana,

   wakaa pamoja nami, 

   wanikaribisha. 

   Unanifurahisha

   kwa wema wako mwingi, 

   sababu hii nakusifu.


4. Maisha yanapita 

   upesi, ni safari 

   ya kwenda mbinguni.

   Unifundishe, Bwana, 

   kuelekea kwako: 

   Pazuri ni mbinguni tu. 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima