192. Nyumba Hubarikiwa
1. Nyumba hubarikiwa ukaamo,
Yesu, uliye mpenzi wa mioyo,
wakukaribishapo kwa furaha,
uliye mgeni wa heshima kuu.
Mioyo yetu inapokupenda
na macho yote yakungojapo,
midomo yote ikuulizapo,
na watu wote wanapokutii.
2. Nyumba hubarikiwa,
mume na mke
wanapopatana kukupenda.
Wakikumbuka, kama wamepewa
wokovu mmoja nawe, ee Yesu.
Wakushikapo na kutegemea,
wakati wa furaha na shida,
wasipoacha njia ya uzima hata
huzuni ikiwashika.
3. Nyumba hubarikiwa,
wawekwamo
watoto wakujue, wakutii.
Uwapendaye na kuwabariki
watoto walio kondoo wako.
Wanapokusanyika wa nyumbani,
wasikilize Neno lako tu,
wanaposhirikiana kuomba
na kukufurahisha, Mwokozi.
4. Nyumba hubarikiwa,
Wewe Bwana,
ukiwa mwenzao furahani,
namo shidani kwani unajua
kuponya na kutuliza mioyo.
Mpaka wamalizapo kazi yako
na kuiacha dunia mwisho,
wafike pale, mwenyewe ulipo
katika nyumba ya Baba yako.
Comments
Post a Comment