212. Bwana Twakuomba Sasa
1. Bwana twakuomba sasa,
tutokee sisi hapa,
kwani siku yako leo.
Tupe, kufikiri vema
Neno lako la uzima,
na la ukombozi wetu
sisi tuliopotea
tupate kurudi kwako.
2. Yawe mbali kwetu sasa
kila mambo masumbufu.
Roho na mioyo yetu
ikaongee na Mungu.
Tupate kutiwa hamu
ya raha iliyo kwako,
itakayotutokea
baada ya maisha haya.
3. Naona kitini pako
taji lao washindao;
nasikia nyimbo zao
waishao kupigana.
Hao wakusifu wewe
kwa zaburi na kwa shangwe.
Hata mimi nijalie
nipate kufika kule.
4. Upungufu wangu wote
ufunike wewe Bwana;
niwe mtakatifu wako
duniani hapa chini,
nisikose kuingia
furahani kwa wageni,
uliowaita wewe
kuimba nyimbo za shangwe.
Comments
Post a Comment