221. Ee Bwana Mungu Mkuu
1. Ee Bwana Mungu Mkuu
uliye muumbaji,
Yesu uliye mwenye fahari,
ninajitolea sasa na milele
nakupa roho na mwili wangu
maisha yangu nakupa wewe,
vyote na vyote vilivyo vyangu,
ninakutolea kwa furaha.
2. Mionzi ya jua
na mwanga wa mwezi
vyatoka nuruni mwako Yesu.
Na jeshi la nyota
ndilo taji zuri
kichwani kwako
Mfalme wa mbingu.
Vyote na vyote ulimwenguni
asili yao kwako ee Yesu;
vyote vyahubiri ukuu wako.
3. Umechaguliwa kuwa kimbilio
la watu wenye shida na
dhambi.
We wasaidia, dhambi waondoa,
japo mashaka yakiwa mengi,
hatari zote watukingia.
Jeshi la adui utalishinda
kwa nguvu yako kuu
ya kimbingu.
4. Toka duniani twakuelekezea
macho yatamani.
Mfalme Yesu.
Sisi tu gizani, Nawe u nuruni,
utuangaze mioyo yetu.
Uthibitishe mwenendo wetu,
ili mwishoni tusikukose,
tufike wote mbinguni juu.
Comments
Post a Comment