166. Wamwendea Yesu
1. Wamwendea Yesu
kwa kusafishwa,
na kuoshwa
kwa damu ya Kondoo?
Je neema yake umemwagiwa?
Umeoshwa
kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
itutakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe
mno: Umeoshwa
kwa damu ya Kondoo?
2. Wamwandama daima
Mkombozi na kuoshwa
kwa damu ya Kondoo?
Je, waishi kwake msulibiwa?
Umeoshwa
kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa …
3. Atakapokuja Bwana arusi
uwe safi kwa damu ya kondoo.
Yafae kwenda Mbinguni mavazi
yafuliwe kwa damu ya kondoo.
Kuoshwa …
4. Yatupwe yaliyo na takataka,
na uoshwe
kwa damu ya Kondoo.
Huoni kijito chatiririka
na uoshwe kwa damu ya
Kondoo?
Kuoshwa …
Comments
Post a Comment