159. Mbinguni, Mbinguni
1. Mbinguni, mbinguni
kuna mji mwema.
/: Wapendeza sana,
ni wake Mungu. :/
2. Milango ya mjini ni dhahabu tu,
/: Mungu ndiye jua
anaung’aza. :/
3. Ugonjwa hauko, kufa hakuna.
/: Wenyeji wa humo ni
wa kweli tu :/
4. Waimba usiku hata na mchana
/: Wakimsifu Bwana
Mungu wetu tu. :/
5. Wote waimbao wana furaha.
/: Wang’azwa na damu
ya Bwana Yesu. :/
6. Vijana sikieni wote kwamba.
/:Twapendwa na Yesu,
Bwana wa mbingu. :/
7. Twendeni kuingia wote mjini,
/: Tupewe uzima na
Bwana wetu! :/
Comments
Post a Comment