189. Uuchunguze Ndani Yangu

1.  Uchunguze ndani yangu, 

    iwe safi nia,

    kwangu kama kwako

    Mungu, idhihiri pia.


2.  Uchunguze moyo wangu 

    unifunulie, 

    yaliyomo ndani yangu, 

    nami niyajue.


3.  Kwanza washa zako tambi,

    kumefunga giza,

    nijue ambavyo dhambi

    ni ya kuchukiza.


4.  Uchunguze na mawazo,

    ni mbegu za mambo. 

    Asili ya machukizo, 

    maumbuo umbo.


5.  Uzidi kuyachunguza

    katikati yangu.

    Hata uishe nifundisha 

    udhaifu wangu. 


6.  Hapo nikikuinamia 

    mbele zako Mungu,

    hakika nitakujua 

    ndiwe mpenzi wangu.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima