190. Onjeni, Onjeni
1. K: Onjeni, onjeni.
W: Onjeni, muone kuwa
Bwana ni mwema,
onjeni.
K: Heri.
W: Anayemtumaini,
K: Heri
W: Anayemtumaini,
ni heri
2. K: Mcheni, mcheni.
W: Mcheni Bwana,
mlio watakatifu,
mcheni.
K: Wale
W: Wanaomcha Bwana.
K: Wale
W: Wanaomcha Bwana
ni heri.
3. K: Na simba, na simba.
W: Na simba hutindikiwa,
Huona njaa, na simba.
K: Bali
W: Wamtafutao Bwana,
K: Hawa
W: Hawahitaji kitu,
chochote
4. K: Njooni, njooni.
W: Njooni, enyi wanangu,
nisikilize, njooni.
K: Nanyi
W: Mtamjua Bwana,
K: Nanyi
W: Mtamjua Bwana, njooni.
5. K: Ni nani, ni nani?
W: Ni nani apendezwaye
nao uzima, ni nani?
K: Mwenye
W: Kupenda siku nyingi,
K: Mwenye
W: Kupenda siku nyingi
za mema.
6. K: Zuia, zuia.
W: Zuia ulimi, sema
yaliyo kweli, zuia.
K: Hata
W: Midomo bila hila
K: Hata
W: Midomo bila hila, zuia.
7. K: Uache, uache
W: Uache mabaya tenda
mapenzi yake, uache
K: Nawe
W: Utafute amani,
K: Nawe
W: Utafute amani, amani.
Comments
Post a Comment