187. Kama Ulivyoagiza

1.  Kama ulivyoagiza 

    kabla kuuawa, 

    hivi nitafanya, Bwana 

    nitakukumbuka.


2.  Wewe kwa ajili yangu 

    ulitoa mwili

    katika mkate wako huu,

    nitaukumbuka.


3.  Vivyo damu ya thamani

    Wewe ulitoa.

    Katika kikombe hiki, 

    nitaikumbuka.


4.  Nitazamapo Golgota,

    kuona msalaba,

    na kipaji cha kafara 

    nitakikumbuka.


5.  Siwezi kusahau  jinsi 

    ulivyoumia,

    kweli nikiwapo mzima 

    nitakukumbuka.


6.  Kwa hiyo nakungojea 

    Ee Bwana kwa kuwa

    ujapo mara ya pili 

    utanikumbuka.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima