219. Asubuhi na Mapema
1. Asubuhi na mapema nakukaribia,
kukushukuru, ee Bwana,
kwa uzima wangu.
2. Uliyenipa usiku kulala ni mzima,
nakuomba sasa, Mungu,
unilinde mchana.
3. Nilinde majaribuni,
kwani sina nguvu,
hivi leo maovuni
uwe ngao yangu!
4 Katika maneno yangu
nisiseme uongo,
macho yako Bwana Mungu,
yanitunze mimi!
5. Njia yangu nipitayo
wewe uwe nami,
kila niendako leo
uwe kiongozi!
Comments
Post a Comment