230. Mwezi Umechipuka
1. Mwezi umechipuka
na nyota zamulika
mbinguni popote.
Makonde yote kimya,
na kunako mabonde
ukungu mzuri unakaa.
2. Dunia imekuwa
nchi ya utulivu,
ni nyumba ya raha.
Viumbe vyenye taabu,
waume, wake, wana
na watulie usiku.
3. Tukiwa na kiburi,
tu wakosaji sana,
wapuuzi kabisa.
Twatunga vya uongo,
na maarifa yote
yametutenga na Mungu.
4. Utuonyeshe, Mungu,
wokovu wa kikweli,
tusijidanganye!
Tukae duniani
kama watoto wema
wamtegemeao Baba.
5. Na sasa ndugu zangu,
tuende kujilaza
kwa Jina la Mungu.
Atupe usingizi
sisi tuliochoka,
hata majirani wote!
Comments
Post a Comment