236. Neno Lako Bwana Wetu

1. Neno lako Bwana wetu,

   umande wa mioyo, 

   uinyweshe miche yote 

   katika shamba lako. 

   Ikinyweshwa itakua, 

   baadaye itazaa,

   matunda mema sana.


2. Neno lako ni upanga

   linapenya mioyo.

   Ni shoka kali, lachanja 

   kiini na mifupa. 

   Twakuomba; Neno lako

   likomeshe makosa 

   litusafishe sisi.


3. Neno lako Bwana wetu

   ni nyota yenye nuru. 

   Linafundisha wajinga, 

   wajue njia yako.

   Nuru yako itung’aze 

   isizimike kwetu; 

   ila ituangaze.


4. Uwape watu wote njaa 

   ya kusikia Neno. 

   Uwape kiu ya roho 

   walikubali hilo.

   Neno lako lashibisha

   wanaolitumia,

   kuwa chakula chao.


5. Neno lako litangazwe

   katika pande zote,

   utume mitume wengi 

   walihubiri pote

   Uwaamshe walalao 

   walikubali wote

   Neno lenye uzima.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima