235. Ukae Kwetu Bwana
1. Ukae kwetu Bwana
na rehema yako,
Shetani asiweze kutudhuru tena.
2. Ukae kwetu Yesu
na Neno la kweli,
tupate ukombozi tukilifuata.
3. Ukae kwetu nuru
na mwanga wa mbingu,
utuongoze njia iendayo kwako.
4. Ukae kwetu Bwana
mwenye enzi yote,
utupe nguvu nyingi tukutumikie.
5. Ukae kwetu Mponya
na nguvu yako kuu,
adui na dunia wasituharibu.
6. Ukae kwetu Mungu
na ukweli wako,
tusikuache wewe. Utupeleke juu!
Comments
Post a Comment