234. Nifungulie Mlango

1. Nifungulie mlango 

   niingie Sayuni. 

   Ndipo nitakapoona

   raha na furaha kuu. 

   Mwokozi anapokaa 

   Mungu wa utukufu.


2. Nimekuja kwako 

   Bwana, nakusihi: 

   Njoo kwangu.

   Unapochagua wewe 

   pana raha ya kweli.

   Nakupa moyo wangu 

   uwe kikao chako.


3. Unisaidie Bwana, 

   nijiweke tayari,

   nyimbo zangu na maombi 

   yakubalike kwako. 

   Utakase mwili huu 

   uwe wako, Bwanangu.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima