233. Mungu Yupo Hapa
1. Mungu yupo hapa,
na tumsujudie,
tumche tukamtumikie.
Yu pamoja nasi,
nyamazeni wote
Tumwabudu Mungu wetu.
Wanaolitaja
Jina lake, njooni,
tumpeni sadaka.
2. Mungu yupo hapa,
anayesifiwa
na malaika kila siku.
Wote wanaimba:
Mungu Mtakatifu,
aheshimiwe popote.
Ee Mungu sikia
tukikuimbia na sisi wadogo.
3. Twataka kuacha
mambo ya dunia
na uzuri wake wote.
Mioyo na mapenzi
hata nia zetu
tunakutolea Bwana.
Wewe tu, u Mungu,
anayestahili sifa za viumbe.
4. Mwokozi ingia,
mioyo yetu yote,
iwe nyumba yako wewe.
Ndiwe Bwana wetu,
utusaidie
tukupende siku zote.
Tukiwa wako tu
tukae na wewe
tukusujudie!
Comments
Post a Comment