232. Haleluya, Nakusifu
1. Haleluya, nakusifu
Mungu uliyenipa
leo tena siku yako,
ishindayo nyingine,
inanifurahisha
moyo wangu kabisa.
2. Ninaacha masumbuko;
leo siku ya Bwana.
Ninamtumikia Mungu,
kwa nguvu zangu zote.
Leo vyote havifai
ila kazi ya Mungu.
3. Ubariki Neno lako
linapohubiriwa,
liingie mioyoni,
watu wategemee.
Nyimbo hata maombi
yakufikie Mungu.
4. Unisaidie Bwana
nimalize siku hii
kama nilivyoianza
nikikutumikia.
Mwisho nione kwako
sikukuu ya milele.
Comments
Post a Comment