231. Mungu Kanilinda Mimi
1. Mungu kanilinda mimi
kwa wema mpaka leo.
Alinda mwili na roho
usiku hata mchana.
Aniongoza kila saa,
apenda kunibariki
na kunisaidia.
2. Ninakushukuru Mungu
sababu ya rehema,
uliyonifanyizia
Bwanangu siku zote.
Ninakumbuka daima
mambo unitendeayo,
ukanisaidia.
3. Uzidi kunibariki,
kwa wema wako Bwana.
Nisaidie kila saa
na mahali popote.
Nimshike Yesu Mwokozi,
hata na siku ya kufa
nipate mwisho mwema.
Comments
Post a Comment