229. Usiku Uingiapo
1. Usiku uingiapo,
umwaze Mungu Mkuu,
aendeshaye dunia
kwa mwendo mtulivu.
2. Kwa nini wahangaika
usiku na mchana?
Umtwishe huzuni yako
aliyekuumba.
3. Kwake haujapunguka
uwezo na msaada.
Atayatimiza yote
aliyoyaanza.
4. Ukamwachie kutenda
atakalo kwako!
Kwa hiyo ulale raha
na kufurahiwa.
Comments
Post a Comment